Pages - Menu

Wednesday, 20 August 2014

Matukio picha Mke wa Rais alipotembelea Kituo cha watoto cha SOS Dar es salaam ,

Kutoka kushoto  Dilip Musale , Mkurugenzi wa wa kituo Dr.Alex Lengeju wakishuhudia  Mama Salma Kikwete na  mtoto wa SOS ( Innocent Sutta) wakikata keki  wakati Mama Salma Kikwete alipotembelea  katika kituo hicho kilichopo Mwenge jijini Dar es salaam, Mtoto Innocent Sutta ni mtoto mwenye kipaji kutoka katika kituo hicho na amepata nafasi ya kwenda kusoma nchini Ghana.

 Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni
ya Sadolin nchini ambao walijitolea kupaka rangi vijiji vyote vya watoto
yatima hapa nchini.


 Mama Salma kikwete akimlisha keki mtoto mwenye kipaji maalum Innocent Suta kutoka kijiji cha watoto cha SOS 

 Mama Salma Kikwete akipaka rangi katika kituo cha kulelea watoto cha SOS kilichopo Mwenge jijini Dar es salaam.

Mama Salma Kikwete akimwagili mti alioupanda katika kituo hicho wakati alipotembelea kituoni hapo hivi karibuni.

"Asante  SADOLIN  kwa kutungarisha"

Picha kwa Hisani ya  Full shangwe Blog

No comments:

Post a Comment